Al-Baqara
This is a translation of Tafsīr as-Saʿdī as IslamHouse.com publishes it at saadi.islamenc.com, read from that site’s pages. The site does not say who translated it or which printed edition it follows, and states no terms for taking its text, so the right to show it is not verified. Nobody has compared it with a printed book, and no scholar has reviewed it. Each passage stands beside the verses it comments on, which are the Qur’ān text of Tanzil, shown as it is there; a verse the site gives no commentary of its own stands with the passage before it, and the index names each such verse. Sabīl did not write or translate any of it.
Text fromsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)taken 2026-10-22
وَمِنَ ٱلنَّاسِ مَن يَقُولُ ءَامَنَّا بِٱللَّهِ وَبِٱلْيَوْمِ ٱلْـَٔاخِرِ وَمَا هُم بِمُؤْمِنِينَ 8 يُخَـٰدِعُونَ ٱللَّهَ وَٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ وَمَا يَخْدَعُونَ إِلَّآ أَنفُسَهُمْ وَمَا يَشْعُرُونَ 9
Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema katika kuwaeleza wanafiki ambao sura yao ya nje ni Uislamu, lakini ndani yao ni ukafiri:
(8-9) Na jua ya kuwa unafiki ni kuonyesha heri na kuficha shari (maovu). Na unaingia katika huu ufafanuzi unafiki wa kiitikadi (kiimani) na unafiki wa kivitendo. Na unafiki wa kivitendo ni kama ule alioutaja Nabii - rehema na amani ziwe juu yake - katika kauli yake. "Alama za mnafiki ni tatu: Anapozungumza, husema uongo. Na anapoahidi, huvunja ahadi. Na anapoaminiwa, hufanya hiyana.” Na katika riwaya, “Na anapogombana, hupita mipaka (anaacha haki)." Na ama unafiki wa kiitikadi unaomtaoa (mtu) nje ya duara ya Uislamu; ni ule aliowaeleza nao Mwenyezi Mungu wanafiki katika Sura hii na (sura) nyinginezo. Na unafiki haukuwepo kabla ya kuhama kwa Nabii - rehema na amani ziwe juu yake - kutoka Makka kwenda Madina, wala baada ya Hijra, mpaka vilipotokea vita vya Badr, na Mwenyezi Mungu akawapa Waumini ushindi na nguvu, na kadhalilika wale waliokuwa Madina miongoni mwa wale ambao hawakusilimu. Kwa hivyo, baadhi yao wakaudhihirisha Uislamu kwa hofu na kuhadaa, na kwa minajili ya kuhifadhi damu zao, na kufanya mali zao ziwe salama. Basi wakawa miongoni mwa Waislamu walioonekana kwa nje zaidi kuwa wao ni miongoni mwao, lakini kwa hakika wao hawakuwa miongoni mwao. Na kutokana na upole wa Mwenyezi Mungu kwa Waumini ni kwamba aliweka wazi hali zao (yaani wanafiki), na akawaeleza kwa maelezo ambayo wanapambanuka kwayo, ili Waumini wasidanganyike nao, na ili waweze kudidimiza (kuzuia) mengi katika maovu yao. Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: “Wanafiki wanaogopa isije ikateremshwa Sura itakayowatajia yaliyomo katika nyoyo zao.” Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu akawaeleza kuwa wana unafiki asili, akasema: “Na katika watu, wako wasemao: Tumemwamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho, wala wao si wenye kuamini.” Kwa maana, wao kwa hakika husema kwa ndimi zao yasiyokuwa nyoyoni mwao. Basi Mwenyezi Mungu akawakadhibisha kwa kauli yake “wala wao si wenye kuamini.” Kwa sababu, imani ya kweli ni ile ambayo moyo na ulimi vimekubaliana juu yake. Ama huu mwingine, ni kumhadaa tu Mwenyezi Mungu na waja wake Waumini. Na kuhadaa ni mwenye kuhadaa kumdhihirishia kitu yule anayehadaa na anaficha kinyume chake ili aweze kufikia makusudio yake kutoka kwa anayehadaa. Na hawa wanafiki walimchukulia Mwenyezi Mungu na waja wake njia hii, lakini kuhadaa kwao kukawarudia wao wenywe. Na hili kwa hakika ni katika maajabu. Kwa maana, mwenye kuhadaa ima afanikiwe katika kuhadaa kwake na apate kile anachotaka, au asalimike kwa namna ya kwamba si kwa faida yake wala hasara yake. Lakini hawa kuhadaa kwao kuliwarudia wao wenyewe, kama kwamba wanafanya yale wanayofanya katika vitimbi (hila) ili kujiangamiza nafsi zao, na kuzidhuru, na kuzifanyia vitimbi. Kwa sababu, Mwenyezi Mungu Mtukufu hadhuriki kitu na kuhadaa kwao. Nao waja wake Waumini haviwadhuru kitu vitimbi vyao. Kwa hivyo, haiwadhuru Waumini ikiwa wanafiki watadhihirisha imani. Kwa hivyo mali zao zikasalimika kwa hilo, nazo damu zao zikahifadhika, lakini vitimbi vyao vikawafika kwenye koo zao. Na wakapata kudhalilishwa na fedheha kwa sababu ya hilo katika dunia hii, na huzuni yenye kuendelea kwa sababu ya yale wanayopata Waumini ya kuwa na nguvu na ushindi. Kisha huko Akhera watapata adhabu chungu, yenye kuumiza na kuhuzunisha kwa sababu ya uongo wao, ukafiri wao, na uovu wao. Na hali ni kwamba kwa sababu ya ujinga wao na upumbavu wao, hawalitambui hilo.