Al-Baqara
This is a translation of Tafsīr as-Saʿdī as IslamHouse.com publishes it at saadi.islamenc.com, read from that site’s pages. The site does not say who translated it or which printed edition it follows, and states no terms for taking its text, so the right to show it is not verified. Nobody has compared it with a printed book, and no scholar has reviewed it. Each passage stands beside the verses it comments on, which are the Qur’ān text of Tanzil, shown as it is there; a verse the site gives no commentary of its own stands with the passage before it, and the index names each such verse. Sabīl did not write or translate any of it.
Text fromsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)taken 2026-10-22
فَوَيْلٌ لِّلَّذِينَ يَكْتُبُونَ ٱلْكِتَـٰبَ بِأَيْدِيهِمْ ثُمَّ يَقُولُونَ هَـٰذَا مِنْ عِندِ ٱللَّهِ لِيَشْتَرُوا۟ بِهِۦ ثَمَنًا قَلِيلًا ۖ فَوَيْلٌ لَّهُم مِّمَّا كَتَبَتْ أَيْدِيهِمْ وَوَيْلٌ لَّهُم مِّمَّا يَكْسِبُونَ 79
(79) Mwenyezi Mungu Mtukufu aliwaahidi adhabu wale wanaopotosha Kitabu, ambao wanasema kuhusu kuwapotosha kwao na uongo wao. "Hiki kimetoka kwa Mwenyezi Mungu," na hili ndani yake lina kudhihirisha uongo na kuficha haki. Na walifanya hivyo pamoja na kujua kwao "ili wanunue kwacho thamani ndogo." Na dunia nzima tangu mwanzo wake hadi mwisho wake ni thamani ndogo. Hivyo basi, wakaufanya uongo wao kuwa mtego ambao kwa (mtego) huo, wanawinda vilivyo mikononi mwa watu. Basi wakawadhulumu (watu) kwa namna mbili: kwa upande wa kuwachanganyia dini yao, na kwa upande wa kuwachukulia mali zao bila ya haki, bali kwa batili ya batili zote. Na [hilo] ni kubwa zaidi kuliko mwenye kuzichukua kwa nguvu, wizi na mfano wake. Kwa sababu ya hayo, (Mwenyezi Mungu) aliwaahidi adhabu kwa mambo haya mawili akasema, "Basi ole wao kwa yale iliyoyaandika mikono yao." Yani kwa sababu ya kukibadilisha na (kwa sababu ya) uongo. "Na ole wao kwa yale wanayoyachuma." katika mali. Na "wayl" ni adhabu kali na majuto, ambayo miongoni mwake ni ahadi ya adhabu kubwa. Alisema Sheikhul-Islaam alipozitaja Aya hizi kuanzia kauli yake "Je, mnatumai?" hadi (kauli yake) "wanayoyachuma": Hakika Mwenyezi Mungu amewakashifu wale wanaobadilisha maneno (ya Mwenyezi Mungu) kutoka mahali pake. Na hilo anaingia ndani yake yule anayebebesha Kitabu na Sunnah yale aliyoanzisha miongoni mwa uzushi na batili. Na akamkashifu yule asiyejua Kitabu isipokuwa uongo anaoutamani. Na hilo anaingia ndani yake yule aliyeacha kuizingatia Qur-ani, na hakuijua isipokuwa kuzisoma herufi zake tu. Na anaingia ndani yake mwenye kuandika kitabu kwa mkono wake, kinachohalifu Kitabu cha Mwenyezi Mungu ili apate kwacho dunia. Na akasema: Hakika, hiki kimetoka kwa Mwenyezi Mungu, kama vile aseme: Hii ndiyo Sheria na Dini. Na hii ndiyo maana ya Kitabu na Sunnah. Na huku ndiko kufahamu kwa watangulizi wema na maimamu. Na hii ndiyo misingi ya Dini ambayo ni lazima iaminiwe na kila kibinafsi na kijumla. Na anaingia ndani yake mwenye kuficha alichonacho katika Kitabu na Sunnah, ili asije mwenye kumpinga kuichukua kuwa hoja dhidi yake katika haki ambayo anaisema. Na mambo haya ni mengi sana katika watu wa matamanio kijumla, kama vile Ar-rafidhwa [na Al-Jahmiyya na mfano wao miongoni mwa watu wa matamanio na Kalaam (yani wanaotegemea akili zao katika kuthibitisha imani), na katika watu wa matamanio] kila mmoja wao kivyake, kama vile wengi wa wanaojinasibisha na mafaqihi (wanachuoni) ... » mwisho.