Skip to content
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Baqara
Sūrah 2

Al-Baqara

This is a translation of Tafsīr as-Saʿdī as IslamHouse.com publishes it at saadi.islamenc.com, read from that site’s pages. The site does not say who translated it or which printed edition it follows, and states no terms for taking its text, so the right to show it is not verified. Nobody has compared it with a printed book, and no scholar has reviewed it. Each passage stands beside the verses it comments on, which are the Qur’ān text of Tanzil, shown as it is there; a verse the site gives no commentary of its own stands with the passage before it, and the index names each such verse. Sabīl did not write or translate any of it.

Text fromsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)taken 2026-10-22

Verse 236

لَّا جُنَاحَ عَلَيْكُمْ إِن طَلَّقْتُمُ ٱلنِّسَآءَ مَا لَمْ تَمَسُّوهُنَّ أَوْ تَفْرِضُوا۟ لَهُنَّ فَرِيضَةً ۚ وَمَتِّعُوهُنَّ عَلَى ٱلْمُوسِعِ قَدَرُهُۥ وَعَلَى ٱلْمُقْتِرِ قَدَرُهُۥ مَتَـٰعًۢا بِٱلْمَعْرُوفِ ۖ حَقًّا عَلَى ٱلْمُحْسِنِينَ 236

{236} Yani hakuna juu yenu - enyi kundi la waume - ubaya na dhambi kuwataliki wanawake kabla ya kuwagusa, na kuwakatia mahari yao. Na ingawa katika hilo kuna kumvunja, lakini hilo linazibwa kwa kumpa cha kumliwaza. Kwa hivyo, ni juu yenu kuwapa kitu cha kuwaliwaza katika mali, ili kuwapoza fikira zao. "Mwenye wasaa kwa kiwango awezacho na mwenye dhiki kwa kiwango awezacho" na hilo ni linarudi kwa ada, na kwamba inatofautiana kulingana na hali. Na ndiyo maana akasema, "maliwazo kwa wema". Na hii ni haki ya wajibu "juu ya watendao mema". Hawana haki ya kuwapunja. Na kwa vile walivyowafanya watarajie ndoa, na mioyo yao ikafungamana nao, lakini hawakuwapa walichokuwa wakitaka. Basi ni lazima badala ya hayo wawape cha kuwaliwaza. Wallahi! Ni hukumu nzuri hii ya Mwenyezi Mungu, na yenye kuashiriaje hekima ya aliyeiweka kama sheria na rehema zake? Na ni nani aliye bora zaidi katika kuhukumu kuliko Mwenyezi Mungu kwa watu wenye yakini? Na hii ni hukumu ya wanawake waliotalikiwa kabla ya kuguswa, na kabla ya kuwabainishia mahari yao. Kisha akataja hukumu ya wale waliobainishiwa mahari yao, akasema: