Al-Baqara
This is a translation of Tafsīr as-Saʿdī as IslamHouse.com publishes it at saadi.islamenc.com, read from that site’s pages. The site does not say who translated it or which printed edition it follows, and states no terms for taking its text, so the right to show it is not verified. Nobody has compared it with a printed book, and no scholar has reviewed it. Each passage stands beside the verses it comments on, which are the Qur’ān text of Tanzil, shown as it is there; a verse the site gives no commentary of its own stands with the passage before it, and the index names each such verse. Sabīl did not write or translate any of it.
Text fromsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)taken 2026-10-22
فَإِن طَلَّقَهَا فَلَا تَحِلُّ لَهُۥ مِنۢ بَعْدُ حَتَّىٰ تَنكِحَ زَوْجًا غَيْرَهُۥ ۗ فَإِن طَلَّقَهَا فَلَا جُنَاحَ عَلَيْهِمَآ أَن يَتَرَاجَعَآ إِن ظَنَّآ أَن يُقِيمَا حُدُودَ ٱللَّهِ ۗ وَتِلْكَ حُدُودُ ٱللَّهِ يُبَيِّنُهَا لِقَوْمٍ يَعْلَمُونَ 230
{230} Mola Mtukufu anasema: "Na akimtaliki" yani talaka ya tatu, "basi yeye si halali kwake baada ya hayo mpaka aolewe na mume asiyekuwa yeye." Yani nikaha sahihi, halali na amjamii. Kwa sababu, nikaha ya kisheria haiwi isipokuwa ile iliyo halali, na ambayo ina mkataba na kujamiiana. Na haya ndiyo makubaliano ya wanachuoni wote. Na nikaha ya pili ni lazima iwe nikaha ya kutaka kuoa. Na ikiwa itakusudiwa nayo kumhalalisha mwanamke huyo kwa ajili ya yule wa kwanza, basi hiyo sio ndoa wala haitasaidia katika kuhalalisha, wala kujaamii kwa bwana huyo, kwa sababu yeye si mume (wake). Na wa pili akimwoa kwa kutaka, na akamjaamii, kisha akamwacha, na eda yake ikamalizika; "basi hakuna ubaya juu yao." Yani juu ya yule mume na mkewe wa kwanza, "kurejeana" yani wafunge nikaha mpya kwa sababu amefungamanisha kurejea na wao tu. Kwa hivyo, ikaashiria kuwa kuridhiana kunazingatiwa, lakini kwa sharti katika kurejeana huko idhaniwe "kwamba watashikamana na mipaka ya Mwenyezi Mungu." Kwa namna ya kwamba kila mmoja wao ataitekeleza haki ya mwenzake. Na hilo ni ikiwa watajutia ule uhusiano wao uliopita uliosababisha kutengana, na waazimie kuubadilisha kwa uhusiano mwema. Basi hapa, hakuna ubaya wowote juu yao kurudiana. Na maana isiyokuwa ya moja kwa moja ya Aya tukufu ni kwamba, ikiwa hawadhani kuwa watasimamisha mipaka iliyowekwa na Mwenyezi Mungu, kwa namna ya kwamba wanadhani kuwa kuna uwezekano mkubwa kwamba hali iliyopita itabaki. Na ule uhusiano mbaya hautaondoka, basi kuna ubaya juu yao katika hayo. Kwa sababu, mambo yote ikiwa amri ya Mwenyezi Mungu haitasimamishwa ndani yake, na utiifu kwake haukutekelezwa ndani yake; basi siyo halali kuyaendea. Na katika hili kuna dalili ya kuwa mtu anapaswa akitaka kuingia katika jambo miongoni mwa mambo, hasa uongozi mdogo na mkubwa, ajiangalie katika nafsi yake. Akiona katika nafsi yake nguvu juu yake, na akajiamini, basi na aliendee. Vinginevyo, arudi nyuma. Na Mwenyezi Mungu mtukufu alipozibainisha hukumu hizo kubwa, akasema: "Na hii ni mipaka ya Mwenyezi Mungu." Yani sheria zake ambazo aliipima, na akaibainisha, na akaiweka wazi, "anayoibainisha kwa watu wanaojua." Kwa sababu, wao ndio wanaonufaika kwayo, na wanaowanufaisha wengine. Na katika hili kuna katika fadhila za wenye elimu zisizofichika. Kwa sababu, Mwenyezi Mungu Mtukufu alikufanya kubainisha kwake kwa mipaka yake kuwa mahusisi tu kwao (wenye elimu). Na kwamba wao ndio waliokusudiwa na hilo. Na ndani yake kuna kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu anapenda kwamba waja wake wajue mipaka ya yale aliyoyateremsha juu ya Mtume wake, na wayaelewe.