Skip to content
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Baqara
Sūrah 2

Al-Baqara

This is a translation of Tafsīr as-Saʿdī as IslamHouse.com publishes it at saadi.islamenc.com, read from that site’s pages. The site does not say who translated it or which printed edition it follows, and states no terms for taking its text, so the right to show it is not verified. Nobody has compared it with a printed book, and no scholar has reviewed it. Each passage stands beside the verses it comments on, which are the Qur’ān text of Tanzil, shown as it is there; a verse the site gives no commentary of its own stands with the passage before it, and the index names each such verse. Sabīl did not write or translate any of it.

Text fromsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)taken 2026-10-22

Verses 200–202

فَإِذَا قَضَيْتُم مَّنَـٰسِكَكُمْ فَٱذْكُرُوا۟ ٱللَّهَ كَذِكْرِكُمْ ءَابَآءَكُمْ أَوْ أَشَدَّ ذِكْرًا ۗ فَمِنَ ٱلنَّاسِ مَن يَقُولُ رَبَّنَآ ءَاتِنَا فِى ٱلدُّنْيَا وَمَا لَهُۥ فِى ٱلْـَٔاخِرَةِ مِنْ خَلَـٰقٍ 200 وَمِنْهُم مَّن يَقُولُ رَبَّنَآ ءَاتِنَا فِى ٱلدُّنْيَا حَسَنَةً وَفِى ٱلْـَٔاخِرَةِ حَسَنَةً وَقِنَا عَذَابَ ٱلنَّارِ 201 أُو۟لَـٰٓئِكَ لَهُمْ نَصِيبٌ مِّمَّا كَسَبُوا۟ ۚ وَٱللَّهُ سَرِيعُ ٱلْحِسَابِ 202

Kisha Mola Mtukufu akajulisha kuhusu hali za viumbe, na kwamba wote wanamuomba mahitaji yao, na wanamwomba awazuie yenye kuwadhuru, lakini makusudio yao yanatofautiana. Miongoni mwao “kuna wale wanaosema, “Mola wetu Mlezi, tupe duniani” yani anamuomba katika matakwa ya kidunia. Na yale ambayo ni katika matamanio yake, ilhali hana fungu lolote katika Akhera, kwa sababu ya kutoitaka; na akaiweka hima yake katika dunia peke yake. Na miongoni mwao kuna wale wanaomuomba Mwenyezi Mungu kwa manufaa ya Nyumba hizi mbili, na anamhitaji katika mambo ya dini yake na dunia yake. Na kila mmoja kati ya hawa na hao ana fungu la walichochuma na matendo yao. Na Mola Mtukufu atawalipa kulingana na matendo yao, na hima zao, na nia zao malipo yanayozunguka kati ya uadilifu na fadhila, ambayo kwayo anasifiwa sifa kamilifu zaidi na timilifu zaidi. Na katika Aya hii kuna dalili ya kwamba Mwenyezi Mungu anajibu dua ya kila mwombaji, awe Muislamu au kafiri, au mwenye kupindukia mipaka. Lakini jawabu lake kwa dua ya mwenye kumwomba siyo dalili ya mapenzi yake kwake na ukaribu wake kwake, isipokuwa katika matakwa ya Akhera na mambo ya dini. Na kheri inayotakiwa katika dunia hii inaingia ndani yake kila kinachopendwa na mja. Kama vile riziki nyingi, yenye baraka na halali, na mke mwema, na mtoto anayelipendeza jicho lake, na starehe, na elimu yenye manufaa, na matendo mema, na mfano wa hayo; miongoni mwa mahitaji yanayopendwa na yanayoruhusiwa. Na kheri ya Akhera, ambayo ni kusalimika kutokana na adhabu kaburini, na kisimamo, na moto, na kupata radhi za Mwenyezi Mungu, na kupata neema ya kudumu, na kuwa karibu na Mola Mlezi. Kwa hivyo, dua hii ikawa ni ndio dua inayojumuisha zaidi na kamilika zaidi na inayofaa zaidi kupendelewa. Na ndio maana Nabii rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake alikuwa akiiomba sana kwa dua hii, na akahimiza juu yake.