Skip to content
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Baqara
Sūrah 2

Al-Baqara

This is a translation of Tafsīr as-Saʿdī as IslamHouse.com publishes it at saadi.islamenc.com, read from that site’s pages. The site does not say who translated it or which printed edition it follows, and states no terms for taking its text, so the right to show it is not verified. Nobody has compared it with a printed book, and no scholar has reviewed it. Each passage stands beside the verses it comments on, which are the Qur’ān text of Tanzil, shown as it is there; a verse the site gives no commentary of its own stands with the passage before it, and the index names each such verse. Sabīl did not write or translate any of it.

Text fromsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)taken 2026-10-22

Verse 187

أُحِلَّ لَكُمْ لَيْلَةَ ٱلصِّيَامِ ٱلرَّفَثُ إِلَىٰ نِسَآئِكُمْ ۚ هُنَّ لِبَاسٌ لَّكُمْ وَأَنتُمْ لِبَاسٌ لَّهُنَّ ۗ عَلِمَ ٱللَّهُ أَنَّكُمْ كُنتُمْ تَخْتَانُونَ أَنفُسَكُمْ فَتَابَ عَلَيْكُمْ وَعَفَا عَنكُمْ ۖ فَٱلْـَٔـٰنَ بَـٰشِرُوهُنَّ وَٱبْتَغُوا۟ مَا كَتَبَ ٱللَّهُ لَكُمْ ۚ وَكُلُوا۟ وَٱشْرَبُوا۟ حَتَّىٰ يَتَبَيَّنَ لَكُمُ ٱلْخَيْطُ ٱلْأَبْيَضُ مِنَ ٱلْخَيْطِ ٱلْأَسْوَدِ مِنَ ٱلْفَجْرِ ۖ ثُمَّ أَتِمُّوا۟ ٱلصِّيَامَ إِلَى ٱلَّيْلِ ۚ وَلَا تُبَـٰشِرُوهُنَّ وَأَنتُمْ عَـٰكِفُونَ فِى ٱلْمَسَـٰجِدِ ۗ تِلْكَ حُدُودُ ٱللَّهِ فَلَا تَقْرَبُوهَا ۗ كَذَٰلِكَ يُبَيِّنُ ٱللَّهُ ءَايَـٰتِهِۦ لِلنَّاسِ لَعَلَّهُمْ يَتَّقُونَ 187

{187} Mwanzoni mwa kulazimishwa kwa Saumu ilikuwa ni haramu kwa Waislamu usiku baada ya kulala kula, kunywa na kujamiiana. Kwa hivyo, dhiki ikawapata baadhi yao, basi Mwenyezi Mungu Mtukufu akawafanyia wepesi katika hilo, na akaruhusu kula, kunywa, na kujamiiana. Sawa mtu awe alilala au hakulala, kwa sababu walikuwa wanajihini nafsi zao kwa kuacha baadhi ya waliyoamrishwa. “Kwa hivyo amewakubalia toba yenu” kwa kuwakunjulia jambo ambalo - lau si kulikunjua kwake -, basi lingelesababisha dhambi “na akawasamehe” ile hiana iliyotangulia. “Basi sasa,” baada ya ruhusa hii na ukunjufu kutoka kwa Mwenyezi Mungu, “changanyikeni nao” kwa kufanya jimai, kubusu, kugusana, na kadhalika. “Na tafuteni kile alichowaandikia Mwenyezi Mungu.” Yani kusudieni katika kuchanganyika kwenu na wake zenu kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu. Lakini makusudio makubwa zaidi ya kujamiiana tu, nako ni kupata watoto, na kutunza tupu yake na tupu ya mkewe, na kufikia malengo ya ndoa. Na katika yale aliyowaandikia Mwenyezi Mungu ni Lailatul-Qadr (usiku wa cheo) inayoafikiana na usiku za kufunga kwa Ramadhani. Hampaswi kujishughulisha na raha hii mkaiacha na mkaipoteza. Kwa kuwa, raha inaweza kufikiwa baadaye, lakini Usiku wa cheo ukipita, hauwezi kufikiwa tena. “Na kuleni na kunyweni mpaka uwabainikie weupe wa alfajiri kutokana na weusi wa usiku.” Na huu ndio mwisho wa kula, kunywa, na kujamiiana. Na ndani yake kuna kwamba akila, na mfano wake huku ana shaka kuhusu kupambazuka kwa alfajiri, basi hakuna ubaya juu yake. Na ndani yake kuna ushahidi wa kupendekezwa kula daku (suhuur) kwa sababu ya amri hii. Na kuwa inapendekezwa kuichelewesha kwa kuchukua hilo kutoka katika maana ya ruhusa ya Mwenyezi Mungu, na usahilishaji wake kwa waja wake. Na ndani yake pia kuna dalili kwamba inaruhusika apatwe na alfajiri hali ya kuwa ana janaba kutokana na kujamiiana kabla ya kuoga na ikakubalika saumu yake. Kwa sababu, ni lazima kwamba kuruhusu kujamiiana mpaka alfajiri, atapatwa na alfajiri hali ya kuwa ana janaba. Na chenye kulazimu haki ni haki. “Kisha” inapoingia alfajiri, “timizeni saumu.” Yani kujizuia na mambo yenye kufuturisha “mpaka usiku,” nao ni wakati wa kuzama kwa jua. Na kwa kuwa kuruhusiwa jimai katika usiku za Saumu si ruhusa ya ujumla kwa kila mtu, kwani mtu anayefanya Itikafu haruhusiwi hilo. Mwenyezi Mungu alimtoa katika hukumu hiyo. Akasema: “Wala msichanganyike nao hali ya kuwa mmekaa Itikafu Msikitini”. Yani, hali ya kuwa nyinyi mnasifika kwa hilo. Na hii Aya inaashiria sheria ya kufanya itikafu, ambayo ni kukaa msikitini kwa ajili ya kumtii Mwenyezi Mungu [Mtukufu], na kujitoa kukwendea yeye. Na kwamba itikafu haikubaliki isipokuwa msikitini tu. Na faida ya kuitaja misikiti kwa nomino ya pekee katika hii Aya ni kuonyesha kuwa ni ile ile misikiti wanayoijua, ambamo husimamishwa swala tano za kila siku. Na ndani yake pia kuna kwamba kujamiiana ni miongoni mwa yale yenye kuharibu Itikafu. “Hayo” iliyotajwa - ambayo ni kuharamisha kula, kunywa, kujamiiana, na mfano wake miongoni wa yenye kuharibu funga ya Saumu.Na kumharamishia mtu asiyekuwa na udhuru katika kutofunga, na kuharamisha jimai kwa aliye katika itikafu. Na sawa na hayo miongoni mwa yale yaliyoharamishwa ni “mipaka ya Mwenyezi Mungu” ambayo aliwawekea waja wake. Na akawakataza, na akasema: “Basi msiikaribie” nayo ni yenye ufasaha zaidi kuliko kauli yake "Msiifanye." Kwa sababu, kukaribia kunajumuisha kukataza kufanya yaliyoharamishwa yenyewe, na kukataza njia zake zenye kuifikia mipaka hiyo. Na mja ameamrishwa kuacha yaliyo haramu, na kujiweka mbali nayo kabisa kadiri awezavyo, na kuacha kila sababu inayoitaka kuyaendea (yaliyo haramu). Na ama maamrisho, Mwenyezi Mungu anasema kuyahusu “Hii ni mipaka ya Mwenyezi Mungu, basi msiivunje,” kwa hivyo akakataza kuivuka. “Hivyo ndivyo” yani [Mwenyezi Mungu] alivyowabainishia waja wake hukumu hizo zilizotangulia kwa ubainisho mkamilifu kabisa, na akaziweka wazi kwao kwa uwazi mkamilifu kabisa. “Anavyowabainishia Aya (Ishara) zake watu ili wapate kumcha.” Kwani ikiwa watabainikiwa na haki, wataifuata. Na ikiwa watabainikiwa na batili, watajiepusha nayo. Kwa sababu, mtu anaweza kufanya yale yaliyoharamishwa kwa kutojua kwamba ni haramu, na lau kuwa angejua uharamu wake, basi asingefanya. Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu anawabainishia watu ishara zake, hawatabaki na udhuru wowote wala hoja. Basi hilo linakuwa ni sababu ya uchamungu.