Skip to content
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Baqara
Sūrah 2

Al-Baqara

This is a translation of Tafsīr as-Saʿdī as IslamHouse.com publishes it at saadi.islamenc.com, read from that site’s pages. The site does not say who translated it or which printed edition it follows, and states no terms for taking its text, so the right to show it is not verified. Nobody has compared it with a printed book, and no scholar has reviewed it. Each passage stands beside the verses it comments on, which are the Qur’ān text of Tanzil, shown as it is there; a verse the site gives no commentary of its own stands with the passage before it, and the index names each such verse. Sabīl did not write or translate any of it.

Text fromsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)taken 2026-10-22

Verse 138

صِبْغَةَ ٱللَّهِ ۖ وَمَنْ أَحْسَنُ مِنَ ٱللَّهِ صِبْغَةً ۖ وَنَحْنُ لَهُۥ عَـٰبِدُونَ 138

(138) Yani shikamaneni na upakaji rangi wa Mwenyezi Mungu ambao ni Dini Yake, na isimamisheni kusimama kukamilifu kwa matendo yake yote ya dhahiri na ya yaliyofichika, na itikadi zake zote katika nyakati zote ili muwe na upakaji rangi na sifa moja katika sifa zenu. Na ikiwa ni sifa katika sifa zenu, hilo litawaletea kufuata amri zake kwa hiari, na mapenzi, na dini inakuwa asili yenu kama kupaka rangi nguo kamili ambako kumekuwa sifa yake, basi mkapata furaha ya kidunia na ya kiakhera kwa sababu Dini inahimiza maadili mema, matendo mazuri, na mambo ya juu. Ndio maana akasema kwa njia ya mshangao unaofanya akili safi kufikiria. "Na nani aliye mbora wa kupaka rangi kuliko Mwenyezi Mungu?" yani hakuna aliye bora wa kupaka rangi kuliko kupaka rangi kwake. Na ukitaka kujua mfano unaokubainishia tofauti iliyopo kati ya upakaji rangi wa Mwenyezi Mungu, na upakaji rangi usiokuwa huo miongoni mwa upakaji rangi, basi kipime kitu na kinyume chake. Unaonaje katika mja aliyemuamini Mola wake Mlezi imani sahihi iliyomtia unyenyekevu wa moyo na utiifu wa viungo. Basi hajaacha kujipamba kwa kila sifa nzuri na vitendo vizuri, na tabia kamili, na maelezo matukufu. Na anaacha kila sifa mbaya na mbovu, na upungufu. Basi sifa yake ni ukweli katika kauli yake, na kitendo chake na subira, na ustahimilivu, na usafi, na ujasiri, na ukarimu wa kauli na matendo, na kumpenda Mwenyezi Mungu, na kumnyenyekea, na kumhofu na kumtumaini. Basi, hali yake ni ikhlasi kwa mwabudiwa wake, na wema kwa waja wake. Na mpime yeye na mja aliyemkufuru Mola wake Mlezi, na akamkimbia, na akamwelekea asiyekuwa yeye miongoni mwa viumbe na akasifika kwa sifa mbaya mbaya kama vile: Ukafiri, ushirikina, uwongo, khiyana, kupanga vitimbi, kuhadaa, kutokuwa safi, na kuwaudhi viumbe katika kauli yake na vitendo vyake, hivyo akawa hana ikhlasi kwa mwabudiwa wake, wala wema kwa waja wake. Basi itakudhihirikia tofauti kubwa baina yao, na ikubainikie kwamba hakuna [mwenye kupaka rangi] mbora zaidi kuliko kupaka rangi kwa Mwenyezi Mungu. Na ndani yake ni kwamba hakuna aliye mbaya zaidi wa kupaka rangi kuliko yule aliyejipaka rangi siyo kwa dini yake. Na katika kauli yake: "Na sisi ni wenye kumuabudu Yeye tu." Kuna kubainisha kwa huku kupaka rangi. Nako ni kutekeleza misingi hii miwili: Ikhlasi na kumfuata (Mtume). Kwa sababu, ibada ni jina linalojumuisha kila akipendacho Mwenyezi Mungu na anakiridhia katika vitendo na maneno, ya dhahiri na ya ndani (yaliyofichika). Na haiwi hivyo mpaka Mwenyezi Mungu aiweke kuwa sheria kwa ulimi wa Mtume wake. Na ikhlasi ni mja aukusudie uso wa Mwenyezi Mungu peke yake katika matendo hayo. Kwa hivyo, kumtaja kwanza mwathiriwa, inamanisha kuthibiti (kufungia sifa hizo kwake tu), na akasema "Na sisi ni wenye kumuabudu Yeye tu." Kwa hivyo, akawaelezea kwa ismul-fail. {Yani nomino itokanayo na kitenzi, na hapa ni neno 'aabiduun (wenye kumuabudu)} inayoashiria kuimarika na kutulia, ili ionyeshe kuwa wanasifika kwa hilo (la kumwabudu) [na kwamba imekuwa upakaji rangi usiofutika kwao].