Al-Baqara
This is a translation of Tafsīr as-Saʿdī as IslamHouse.com publishes it at saadi.islamenc.com, read from that site’s pages. The site does not say who translated it or which printed edition it follows, and states no terms for taking its text, so the right to show it is not verified. Nobody has compared it with a printed book, and no scholar has reviewed it. Each passage stands beside the verses it comments on, which are the Qur’ān text of Tanzil, shown as it is there; a verse the site gives no commentary of its own stands with the passage before it, and the index names each such verse. Sabīl did not write or translate any of it.
Text fromsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)taken 2026-10-22
أَوَكُلَّمَا عَـٰهَدُوا۟ عَهْدًا نَّبَذَهُۥ فَرِيقٌ مِّنْهُم ۚ بَلْ أَكْثَرُهُمْ لَا يُؤْمِنُونَ 100
(100) Na haya ndani yake kuna kustaajabu, kwa sababu ya wingi wa mikataba yao na kutokuwa kwao na subira katika kuitimiza. Na "kila" inamaanisha kurudia. Hivyo basi, kila ahadi ilipopatikana, matokeo yake yalikuwa kwamba inavunjwa. Ni nini sababu ya hilo? Sababu ni kuwa wengi wao hawaamini. Na kutokuamini kwao ndiko kunawaletea kuvunja ahadi. Na lau kuwa imani yao ingekuwa kweli, wangekuwa kama wale aliosema Mwenyezi Mungu kuwahusu. "Miongoni mwa Waumini, wapo watu wakweli kwa yale waliyomuahidi Mwenyezi Mungu."