An-Nahl
This is a translation of Tafsīr as-Saʿdī as IslamHouse.com publishes it at saadi.islamenc.com, read from that site’s pages. The site does not say who translated it or which printed edition it follows, and states no terms for taking its text, so the right to show it is not verified. Nobody has compared it with a printed book, and no scholar has reviewed it. Each passage stands beside the verses it comments on, which are the Qur’ān text of Tanzil, shown as it is there; a verse the site gives no commentary of its own stands with the passage before it, and the index names each such verse. Sabīl did not write or translate any of it.
Text fromsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)taken 2026-10-22
وَمَآ أَرْسَلْنَا مِن قَبْلِكَ إِلَّا رِجَالًا نُّوحِىٓ إِلَيْهِمْ ۚ فَسْـَٔلُوٓا۟ أَهْلَ ٱلذِّكْرِ إِن كُنتُمْ لَا تَعْلَمُونَ 43
{43} Yeye Mtukufu anamwambia Nabii wake Muhammad - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - "Nasi hatukuwatuma kabla yako isipokuwa watu wanaume" yaani wewe si kitu kipya miongoni mwa Mitume. Kwa maana hatukuwatuma Malaika kabla yako, bali tuliwatuma wanaume wakamilifu, siyo wanawake "tuliowafunulia Wahyi" wenye sheria na hukumu mbalimbali ambazo ni katika fadhila zake na wema wake juu ya waja wake, na Mitume hao hawakuleta chochote wao wenyewe. "Basi waulizeni wenye ukumbusho;" yaani, watu wa vitabu vilivyotangulia "kama nyinyi hamjui" habari za wa mwanzo, na mkatia shaka kwamba je, Mwenyezi Mungu aliwatuma wanaume? Basi waulizeni wenye elimu juu ya hayo. Wale walioteremshiwa Zaburi na hoja zilizo wazi, nao wakazijua na kuzifahamu. Wao wote walikwisha jua kwa uhakika kwamba Mwenyezi Mungu hakutuma isipokuwa wanaume aliowafunulia wahyi miongoni mwa watu wa mijini. Kwa ujumla, aya hii inawasifia watu wenye elimu, na kwamba aina ya elimu ya juu kabisa ni kukijua Kitabu cha Mwenyezi Mungu alichokiteremsha. Kwa maana Mwenyezi Mungu alimuamrisha asiyejua kuwarudia wenye elimu katika matukio yote. Na ndani ya hili kuna kuwasifia wenye elimu kwamba ni waadilifu na kuwatakasa. Kwa maana, Mwenyezi Mungu aliamrisha kuwauliza, na kwamba kwa kufanya hivyo, mjinga anatoka katika lawama. Basi hilo likaonyesha kwamba Mwenyezi Mungu aliwapa amana ya ufunuo wake na uteremsho wake, na kwamba wameamrishwa kujitakasa nafsi zao na kusifika na sifa za ukamilifu.