Skip to content
Tafsir As-Saadi - Swahili · Yusuf
Sūrah 12

Yusuf

This is a translation of Tafsīr as-Saʿdī as IslamHouse.com publishes it at saadi.islamenc.com, read from that site’s pages. The site does not say who translated it or which printed edition it follows, and states no terms for taking its text, so the right to show it is not verified. Nobody has compared it with a printed book, and no scholar has reviewed it. Each passage stands beside the verses it comments on, which are the Qur’ān text of Tanzil, shown as it is there; a verse the site gives no commentary of its own stands with the passage before it, and the index names each such verse. Sabīl did not write or translate any of it.

Text fromsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)taken 2026-10-22

Verse 109

وَمَآ أَرْسَلْنَا مِن قَبْلِكَ إِلَّا رِجَالًا نُّوحِىٓ إِلَيْهِم مِّنْ أَهْلِ ٱلْقُرَىٰٓ ۗ أَفَلَمْ يَسِيرُوا۟ فِى ٱلْأَرْضِ فَيَنظُرُوا۟ كَيْفَ كَانَ عَـٰقِبَةُ ٱلَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ ۗ وَلَدَارُ ٱلْـَٔاخِرَةِ خَيْرٌ لِّلَّذِينَ ٱتَّقَوْا۟ ۗ أَفَلَا تَعْقِلُونَ 109

{109} Kisha Yeye Mtukufu akasema: "Na hatukuwatuma Mitume kabla yako isipokuwa wanaume;” yaani, hatukutuma Malaika wala wasiokuwa wao miongoni mwa aina mbalimbali za viumbe. Basi kwa nini kaumu yako wanastaajabu jambo la kukutuma wewe na wanadai kuwa wewe huna ubora wowote juu yao, basi una mfano mzuri kutoka kwa Mitume wa kabla yako, "tuliowafunulia wahyi miongoni mwa watu wa mijini.” Yaani, siyo kutoka kwa wakazi wa jangwani, lakini kutoka kwa wakazi wa mijini, ambao ndio wana akili kamili zaidi na maoni mazuri, na ili hali yao ibainike na hali yao iwe wazi. "Je, hawakutembea katika ardhi” ikiwa hawasadiki kauli yako, “wakaona jinsi ulivyokuwa mwisho wa wale waliokuwa kabla yao?” Jinsi Mwenyezi Mungu alivyowaangamiza kwa sababu ya kukadhibisha kwao. Basi jihadharini kuendelea na yale waliyoendelea kuyafanya, yakawapata yale yaliyowapata. "Na hakika nyumba ya Akhera;” yaani, Pepo na vyote vilvyomo miongoni mwa starehe za kudumu "ndiyo bora kwa wamchao Mungu” katika kutekeleza amri zake na kujiepusha na makatazo yake. Kwa maana starehe za dunia zina mipaka, ni dhiki, na ni za kukatika, ilhali starehe za Akhera ni timilifu, kamili na hazina mwisho abadan bali zitaongezeka daima na kuendelea. Hicho ni kipawa kisicho na ukomo. "Basi hamtumii akili?” Yaani, mkayapendelea yale yaliyo bora kuliko yaliyo duni zaidi?