Hud
This is a translation of Tafsīr as-Saʿdī as IslamHouse.com publishes it at saadi.islamenc.com, read from that site’s pages. The site does not say who translated it or which printed edition it follows, and states no terms for taking its text, so the right to show it is not verified. Nobody has compared it with a printed book, and no scholar has reviewed it. Each passage stands beside the verses it comments on, which are the Qur’ān text of Tanzil, shown as it is there; a verse the site gives no commentary of its own stands with the passage before it, and the index names each such verse. Sabīl did not write or translate any of it.
Text fromsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)taken 2026-10-22
وَإِلَىٰ مَدْيَنَ أَخَاهُمْ شُعَيْبًا ۚ قَالَ يَـٰقَوْمِ ٱعْبُدُوا۟ ٱللَّهَ مَا لَكُم مِّنْ إِلَـٰهٍ غَيْرُهُۥ ۖ وَلَا تَنقُصُوا۟ ٱلْمِكْيَالَ وَٱلْمِيزَانَ ۚ إِنِّىٓ أَرَىٰكُم بِخَيْرٍ وَإِنِّىٓ أَخَافُ عَلَيْكُمْ عَذَابَ يَوْمٍ مُّحِيطٍ 84
84. Yaani, "Na" tulituma "kwa watu wa Madyana" nalo ni kabila mashuhuri, ambao walikuwa wakiishi huko Madyana, katika pande za chini kabisa za Palestina, "ndugu yao" kwa nasaba "Shu'aib" kwa sababu walikuwa wanamjua, na wanaweza kujifunza kutoka kwake. Basi akawaambia, "Enyi kaumu yangu! Muabuduni Mwenyezi Mungu. Nyinyi hamna Mungu yoyote isipokuwa Yeye." Yaani, muabuduni yeye tu, kwa maana walikuwa wakimshirikisha, na walikuwa pamoja na ushirikina wao huo wakipunja katika vipimo na mizani, na ndio maana akawakataza kufanya hivyo. Akasema: "wala msipunguze vipimo na mizani;" bali vitimizeni vipimo na mizani kwa uadilifu. "Mimi ninawaona mmo katika hali njema;" yaani, mko katika neema nyingi, na afya nzuri, na mali nyingi, na watoto. Basi mshukuruni Mwenyezi Mungu kwa hayo aliyowapa, wala msiikanushe neema ya Mwenyezi Mungu, akajaiondoa kwenu. "Nami ninawahofia adhabu ya Siku kubwa hiyo itakayowazunguka." Yaani, adhabu itakayowazunguka wala haitaacha yeyote mwenye kubakia.