Hud
This is a translation of Tafsīr as-Saʿdī as IslamHouse.com publishes it at saadi.islamenc.com, read from that site’s pages. The site does not say who translated it or which printed edition it follows, and states no terms for taking its text, so the right to show it is not verified. Nobody has compared it with a printed book, and no scholar has reviewed it. Each passage stands beside the verses it comments on, which are the Qur’ān text of Tanzil, shown as it is there; a verse the site gives no commentary of its own stands with the passage before it, and the index names each such verse. Sabīl did not write or translate any of it.
Text fromsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)taken 2026-10-22
فَقَالَ ٱلْمَلَأُ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ مِن قَوْمِهِۦ مَا نَرَىٰكَ إِلَّا بَشَرًا مِّثْلَنَا وَمَا نَرَىٰكَ ٱتَّبَعَكَ إِلَّا ٱلَّذِينَ هُمْ أَرَاذِلُنَا بَادِىَ ٱلرَّأْىِ وَمَا نَرَىٰ لَكُمْ عَلَيْنَا مِن فَضْلٍۭ بَلْ نَظُنُّكُمْ كَـٰذِبِينَ 27
{27} "Basi wakasema wakuu waliokufuru katika kaumu yake." Yaani watukufu na viongozi wakiukataa wito wa Nuhu, amani iwe juu yake, kama ilivyokuwa desturi ya mfano wao baada yao kwamba wao ndio waliokuwa wa kwanza kukataa wito wa Mitume, “Hatukuoni wewe isipokuwa ni mtu tu mfano wetu" na hiki ni kizuizi dhidi ya kumfuata kulingana na madai yao ingawa katika jambo hilo lenyewe ndilo lililo sahihi ambalo halifai linginelo. Kwa sababu wanadamu wenzake wanaweza kujifunza kutoka kwake na kutafuta ushauri wake katika kila jambo, tofauti na malaika. "Wala hatukuoni wamekufuata isipokuwa wale wetu walio duni." Yaani, hatuoni yeyote miongoni mwetu akikufuata isipokuwa wadhalilifu watu duni sana - kulingana na madai yao - na kiuhakika wao ndio watukufu na watu wenye akili, ambao waliifuata haki, na hawakuwa kama watu wadharauliwao ambao wanaitwa 'wakuu' ambao walimfuata kila shetani aliyeasi, na wakajichukulia miungu ya mawe na miti wakijikurubisha kwayo na wakiisujudia. Je, unadhani kuna mdharauliwa zaidi kuliko hao walio duni mno? Na kauli yao: "Watu wasiokuwa na maoni;" yaani, walikufuata tu bila ya kufikiria wala kuangalia. Bali mara tu ulipowaita, wakakufuata. Wanachomaanisha kwa hayo ni kuwa hao hawana ufahamu wa mambo yao, lakini hawakujua kwamba haki iliyo wazi zinaita kwayo akili za kawaida, na mara tu inapowafikia wenye ufahamu mkubwa, wanaijua na wanaithibitisha. Si kama mambo yaliyofichikana ambayo yanahitaji kuyaangalia na kutafakari kwa kurefu. "Wala hatuwaoni nyinyi kuwa mna ubora wowote kutushinda sisi." Yaani, nyinyi si bora kutuliko ili tuwafuate. "Bali tunawadhania nyinyi kuwa ni waongo." Lakini walisema uongo katika kauli yao hii. Kwa maana, waliona ishara nyingi ambazo Mwenyezi Mungu alimuunga mkono Nuhu kwazo jambo ambalo linalowahitaji wawe na uhakika kabisa juu ya ukweli wake.