মূল অংশে যান
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Baqara
সূরা ২

Al-Baqara

এটি আস-সা‘দীর তাফসীরের একটি অনুবাদ, IslamHouse.com যেভাবে saadi.islamenc.com-এ প্রকাশ করে, সেই সাইটের পাতা থেকে পড়া। সাইটটি বলে না কে এটি অনুবাদ করেছেন বা এটি ছাপা কোন সংস্করণ অনুসরণ করে, এবং এর পাঠ নেওয়ার কোনো শর্তও জানায় না, তাই এটি দেখানোর অধিকার যাচাই করা হয়নি। কেউ এটিকে ছাপা বইয়ের সঙ্গে মেলায়নি এবং কোনো আলেম এটি পর্যালোচনা করেননি। প্রতিটি অংশ যে আয়াতগুলোর উপর মন্তব্য করে তার পাশে আছে; আয়াতগুলো Tanzil-এর কুরআনের পাঠ, সেখানে যেমন আছে তেমন দেখানো; যে আয়াতের জন্য সাইটটি আলাদা কোনো ব্যাখ্যা দেয় না, সেটি তার আগের অংশের সঙ্গে থাকে, আর সূচি এমন প্রতিটি আয়াতের নাম করে। সাবীল এর কিছুই লেখেনি বা অনুবাদ করেনি।

পাঠ নেওয়া হয়েছেsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22-এ নেওয়া

আয়াত ১৯৭

ٱلْحَجُّ أَشْهُرٌ مَّعْلُومَـٰتٌ ۚ فَمَن فَرَضَ فِيهِنَّ ٱلْحَجَّ فَلَا رَفَثَ وَلَا فُسُوقَ وَلَا جِدَالَ فِى ٱلْحَجِّ ۗ وَمَا تَفْعَلُوا۟ مِنْ خَيْرٍ يَعْلَمْهُ ٱللَّهُ ۗ وَتَزَوَّدُوا۟ فَإِنَّ خَيْرَ ٱلزَّادِ ٱلتَّقْوَىٰ ۚ وَٱتَّقُونِ يَـٰٓأُو۟لِى ٱلْأَلْبَـٰبِ ১৯৭

Mola Mtukufu anajulisha kwamba, "Hija" iko ndani ya "miezi maalumu.” Kwa wale walioongeleshwa kiasi kwamba haihitajiki kubainisha, kama vile Saumu ilivyohitajika kubainishwa mwezi wake, na kama vile Mwenyezi Mungu alivyobainisha nyakati za zile swala tano (za kila siku). Ama Hijja, hiyo ilikuwa katika mila ya Ibrahim, ambayo bado haikuacha kuendelea katika kizazi chake, na yenye kujulikana kati yao. Na kilichokusudiwa na miezi maalumu kwa wengi wa wanachuoni ni Shawwal, Dhul-Qa’da, na siku kumi (za mwanzo) katika Dhul-Hijja. Hiyo ndiyo ambayo Ihraam ya Hijja huwa mara nyingi. “Basi anayehirimia Hijja ndani yake (miezi hiyo)," yani alitia nia ya Hijja (Ihraam) ndani yake. Kwa sababu, kuianza tu, kunaifanya kuwa lazima, hata kama ni sunna. Shafii na wale waliomfuata waliitumia Aya hii kama dalili kwamba hairuhusiki kutia nia ya Hija (Ihraam) kabla ya miezi yake. Nikasema: Lau kuwa itasemwa: Ndani yake (aya hii) kuna dalili ya kauli ya wengi wa wanachuoni kwamba ni sahihi kuhirimia [Hijja] kabla ya miezi yake, basi ingekuwa karibu (na usawa). Kwa maana, kauli yake: “Basi anayehirimia Hijja ndani yake (miezi hiyo)” ni dalili ya kwamba kuhirimia kunaweza kuwa au kunaweza kutokuwa ndani yake. Vinginevyo, hangezuilia hilo (la kuhirimia) ndani yake. Na kauli yake: “Basi asijamiiane wala asipindukie mipaka wala asibishane katika Hija.” Yani ni lazima muiheshimu nia ya kufanya Hija (Ihraam) hususan ile inayofanyika katika miezi yake. Na muilinde kutokana na kila chenye kuiharibu au kuipunguza, kama vile kujamiiana na vitangulizi vyake vya kimatendo na kimaneno; hususan mbele ya wanawake wanapokuwepo. Na Fusuuq ni kila maasia, ambayo ndani yake ni makatazo ya ihraam. Na Al-jidaal ni mabishano, mavutano, na mashindano kwa sababu yanasababisha shari (maovu) na huleta uadui. Na makusudio ya Hijja ni kudhalilika na kuvunjika mbele ya Mwenyezi Mungu, na kujikurubisha kwake iwezekanavyo kwa ibada mbalimbali, na kujiepusha na kufanya maovu. Kwa sababu kwa hayo, inakuwa (Hijja) iliyokubaliwa. Na Hija iliyokubaliwa haina malipo isipokuwa Pepo. Na mambo haya, hata ikiwa yameharamishwa katika kila sehemu na wakati, yameharamishwa vikali katika Hijja. Na jua ya kwamba haitimii kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu kwa kuacha madhambi peke yake mpaka atekeleze maamrisho. Na kwa sababu hii, Mola Aliyetukuka akasema: “Na chochote mnachokifanya katika kheri, Mwenyezi Mungu anaijua.” Na alitumia ‘katika’ hapa ili kuonyesha ujumla wa hilo. Kwani, kila kheri, kujikurubisha, na ibada vinaingia katika hilo. Yani kwa hakika Mwenyezi Mungu anajua hilo. Na hili linajumuisha kuwahimiza kukubwa mno juu ya matendo mema, hasa katika sehemu hii tukufu na matakatifu ya hali ya juu. Kwani inafaa kufanya kwa bidii yale anayoweza kufanya, kama vile swala, saumu, sadaka, kuizunguka Al-Ka’ba, kufanya wema kwa maneno na matendo. Kisha Mola Mtukufu akaamrisha kuchukua masurufu kwa ajili ya safari hii yenye baraka. Kwa maana, kuchukua masurufu ndani yake ni kujitosheleza na viumbe, na kuachana na mali zao, kwa kuziomba na kuzitaka kwa uchu. Na kuichukua kwa wingi kuna manufaa na kuna kuwasadia wasafiri, na kunaongeza kujikurubisha kwa Mola Mlezi wa walimwengu. Na masurufu haya ambayo yamekusudiwa kumpa nguvu katika mwili na kumsaidia kufika anakokwenda na kurejea. Na ama masurufu ya kweli yanayoendelea kumnufaisha mwenyewe katika dunia yake na akhera yake, basi ni masurufu ya uchamungu. Ambao (uchamungu huo) ni masurufu ya kwenda katika makazi ya daima. Nayo ndiyo yenye kufikisha kwenye ladha kamili zaidi; na neema nzuri zaidi yenye kudumu milele. Na mwenye kuyaacha masurufu haya, basi huyo ndiye aliyekatikiwa. Ambaye ana uwezekano mkubwa wa kupatwa na kila shari (maovu); na anayezuiliwa kufika kwenye nyumba ya wachamungu. Na huku ni ya uchamungu. Kisha akawaamrisha hilo wenye akili, akasema: “Na nicheni Mimi, enyi wenye akili na busara,” yani enyi watu wenye akili ya kina, mcheni Mola wenu Mlezi ambaye kumcha ndiko kikubwa mno ambacho akili zinaamrisha. Na kuiacha ni dalili ya ujinga na upotovu wa rai.