মূল অংশে যান
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Baqara
সূরা ২

Al-Baqara

এটি আস-সা‘দীর তাফসীরের একটি অনুবাদ, IslamHouse.com যেভাবে saadi.islamenc.com-এ প্রকাশ করে, সেই সাইটের পাতা থেকে পড়া। সাইটটি বলে না কে এটি অনুবাদ করেছেন বা এটি ছাপা কোন সংস্করণ অনুসরণ করে, এবং এর পাঠ নেওয়ার কোনো শর্তও জানায় না, তাই এটি দেখানোর অধিকার যাচাই করা হয়নি। কেউ এটিকে ছাপা বইয়ের সঙ্গে মেলায়নি এবং কোনো আলেম এটি পর্যালোচনা করেননি। প্রতিটি অংশ যে আয়াতগুলোর উপর মন্তব্য করে তার পাশে আছে; আয়াতগুলো Tanzil-এর কুরআনের পাঠ, সেখানে যেমন আছে তেমন দেখানো; যে আয়াতের জন্য সাইটটি আলাদা কোনো ব্যাখ্যা দেয় না, সেটি তার আগের অংশের সঙ্গে থাকে, আর সূচি এমন প্রতিটি আয়াতের নাম করে। সাবীল এর কিছুই লেখেনি বা অনুবাদ করেনি।

পাঠ নেওয়া হয়েছেsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22-এ নেওয়া

আয়াত ১০২–১০৩

وَٱتَّبَعُوا۟ مَا تَتْلُوا۟ ٱلشَّيَـٰطِينُ عَلَىٰ مُلْكِ سُلَيْمَـٰنَ ۖ وَمَا كَفَرَ سُلَيْمَـٰنُ وَلَـٰكِنَّ ٱلشَّيَـٰطِينَ كَفَرُوا۟ يُعَلِّمُونَ ٱلنَّاسَ ٱلسِّحْرَ وَمَآ أُنزِلَ عَلَى ٱلْمَلَكَيْنِ بِبَابِلَ هَـٰرُوتَ وَمَـٰرُوتَ ۚ وَمَا يُعَلِّمَانِ مِنْ أَحَدٍ حَتَّىٰ يَقُولَآ إِنَّمَا نَحْنُ فِتْنَةٌ فَلَا تَكْفُرْ ۖ فَيَتَعَلَّمُونَ مِنْهُمَا مَا يُفَرِّقُونَ بِهِۦ بَيْنَ ٱلْمَرْءِ وَزَوْجِهِۦ ۚ وَمَا هُم بِضَآرِّينَ بِهِۦ مِنْ أَحَدٍ إِلَّا بِإِذْنِ ٱللَّهِ ۚ وَيَتَعَلَّمُونَ مَا يَضُرُّهُمْ وَلَا يَنفَعُهُمْ ۚ وَلَقَدْ عَلِمُوا۟ لَمَنِ ٱشْتَرَىٰهُ مَا لَهُۥ فِى ٱلْـَٔاخِرَةِ مِنْ خَلَـٰقٍ ۚ وَلَبِئْسَ مَا شَرَوْا۟ بِهِۦٓ أَنفُسَهُمْ ۚ لَوْ كَانُوا۟ يَعْلَمُونَ ১০২ وَلَوْ أَنَّهُمْ ءَامَنُوا۟ وَٱتَّقَوْا۟ لَمَثُوبَةٌ مِّنْ عِندِ ٱللَّهِ خَيْرٌ ۖ لَّوْ كَانُوا۟ يَعْلَمُونَ ১০৩

(102-103) Vile vile, Mayahudi hawa walipokitupa Kitabu cha Mwenyezi Mungu, wakawafuata mashetani wale; na walikuwa wakisoma na kuzua uchawi katika ufalme wa Sulaiman, wakati mashetani walipowatolea watu uchawi. Na wakadai kuwa Sulaiman, amani iwe juu yake alikuwa akiutumia, na kwa sababu yake alipata ufalme mkubwa. Nao ni waongo katika hilo. Sulaiman hakuutumia, bali Mkweli alimtakasa katika kauli yake: "Na wala Suleiman hakukufuru" yani kwa kujifunza uchawi, wala hakuifunza, "bali mashetani ndio waliokufuru" katika hilo "wakiwafundisha watu uchawi"; kutokana na kupotosha kwao na pupa yao ya kuwapoteza wanadamu. Na hali kadhalika, Mayahudi waliufuata uchawi ulioteremshwa kwa Malaika wawili waliokuwa katika mji wa Babeli katika nchi ya Iraqi. Waliteremshiwa uchawi kama mtihani na majaribio kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa waja wake. Basi wakawa wanawafundisha uchawi, "Wala hao hawakumfundisha yeyote mpaka" wamnasihi na "wamwambie: Hakika sisi ni mtihani; basi usikufuru." yani usijifunze uchawi; kwa maana ni ukafiri. Kwa hivyo, wanamkataza uchawi na kumpa habari juu ya daraja yake. Hivyo, mashetani kufundisha (watu) uchawi ni kwa njia ya ulaghai na kupotosha, na kuunasibisha na kuueneza kwa yule ambaye Mwenyezi Mungu alimtakasa kutokana na hilo, naye ni Sulaiman amani iwe juu yake. Na kufundisha kwa wale Malaika wawili kulikuwa mtihani pamoja na kumpa nasaha ili wasiwe na hoja. Basi hawa Mayahudi wanafuata uchawi ambao mashetani waliusoma, na uchawi ambao wale Malaika wawili waliufundisha. Hivyo basi, wakaacha elimu ya Manabii na Mitume, na wakaielekea elimu ya mashetani. Na kila mmoja anamili kwa yale yanayomfaa. Kisha akataja maovu ya uchawi, akasema "Wakajifunza kwa hao wawili (Malaika wa Babeli) yale ya kumfarikisha mtu na mkewe." Pamoja na kwamba mapenzi ya wanandoa wawili hayawezi kulinganishwa na mapenzi ya wasio kuwa wao. Kwa sababu Mwenyezi Mungu amesema juu yao "Na akaweka baina yenu mapenzi na huruma” Na katika hilo kuna dalili ya kwamba uchawi una uhakika, na kwamba unadhuru kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, yani kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu. Na idhini ni aina mbili: idhini iliyokwisha pangwa, ambayo inahusiana na matakwa ya Mwenyezi Mungu, kama ilivyo katika Aya hii. Na idhini ya kisheria, kama ilivyo katika kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu katika Aya iliyotangulia "basi huyo ndiye aliyeiteremsha (Qur-ani) moyoni mwako kwa idhini ya Mwenyezi Mungu". Na katika Aya hii na mfano wake kuna kwamba mwanadamu hata akifika nguvu kiasi gani katika kuathiri, basi (hizo nguvu) zinafuata makadirio na amri ya Mwenyezi Mungu, hazijitegemei katika kuathiri. Na hakuna yeyote katika madhehebu ya umma aliyehalifu msingi huu isipokuwa Al-Qadariyya kuhusiana na vitendo vya Mwenyezi Mungu. Wao walidai kwamba vinajitegemea wala havifuati mapenzi ya Mwenyezi Mungu; kwa hivyo wakavitoa nje ya uwezo wa Mwenyezi Mungu. Basi wakawa wamehalifu kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunna za Mtume wake na Ijmaa (makubaliano) ya Maswahaba na wafuatilizi wao. Kisha akataja kuwa elimu ya uchawi ni yenye madhara matupu, na hakuna manufaa yoyote ndani yake, sio ya kidini wala ya kidunia, kama vile yanavyopatikana baadhi ya manufaa ya kidunia katika baadhi ya madhambi. Kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu kuhusu pombe na kamari; "Sema: Katika hivyo (pombe na kamari) zipo dhambi kubwa na manufaa kwa watu. Lakini dhambi zake ni kubwa zaidi kuliko manufaa yake." Na uchawi huu ni wenye madhara matupu, na wala hauhitajiki hata kidogo. Kwani makatazo yote ima yana madhara matupu au ubaya wake ni mkubwa kuliko heri yake. Kama vile maamrisho pia ima yana faida tupu au heri yake ni nyingi zaidi ya ubaya wake. "Na hakika walikwisha jua" yani Mayahudi "kwamba mwenye kuununua " yani kuutaka uchawi kama vile mnunuzi anavyotaka bidhaa "hatakuwa na fungu lolote katika Akhera." Yani mgao, bali inalazimu aadhibiwe. Kwa sababu, kitendo hicho chao sio kwamba walifanya hivyo kwa kutojua, lakini walipendelea maisha ya dunia kuliko ya Akhera. Basi ni kiovu mno "walichouza kwacho nafsi zao, laiti wangelikuwa wanajua" elimu yenye kuzaa matendo, basi hawangeufanya.